• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika watoa mwito wa kuunganisha mikakati ya afya ya umma kwenye maswala ya usalama

    (GMT+08:00) 2018-01-19 08:58:04

    Baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika jana lilijadili matishio ya usalama wa afya yanayozikabili nchi za Afrika.

    Baraza limekubaliana kuwa na mkakati wa pamoja na kituo cha kudhibiti na kinga ya magonjwa cha Afrika (Africa CDC), ili kukabiliana na milipuko ya magonjwa ya kuambukiza, usugu wa vimelea na kupambana na tishio la magonjwa yasio ya kuambukiza.

    Mkurugenzi wa Africa CDC Bw John Nkengasong, ametaka kuwepo kwa mpango wa kushirikisha sekta zote na kuwepo kwa ushirikiano wa kimkakati kupambana na tishio la magonjwa na kulilinda bara la Afrika.

    Baraza hilo limekumbusha madhara ya mlipuko wa Ebola barani Afrika uliolazimu wanajeshi kutumwa mitaani kulinda amani na usalama.

    Bara la Afrika limetajwa kukabiliwa na tishio kuwa usugu wa vimelea dhidi ya dawa za kuua vijidudu, unakadiriwa kusababisha vifo milioni 1.4 kwa mwaka, na kutarajiwa kuligharimu bara hilo hasara ya dola trilioni 42 hadi kufikia mwaka 2050.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako