• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa aonya kuhusu ongezeko la tishio la silaha za maangamizi

    (GMT+08:00) 2018-01-19 08:58:22

    Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Bw. Antonio Guterres ameonya kuwa tishio la kuwepo kwa silaha za maangamizi linaonekana kuchukua kasi duniani kwa sasa.

    Akiongea kwenye mkutano wa baraza la usalama la umoja wa mataifa kuhusu silaha za maangamizi, Bw. Guterres amesema wasiwasi kuhusu silaha za nyuklia kwa sasa uko juu sana kuliko katika kipindi chochote tangu mwisho wa vita baridi, hali ya kuaminiana kati ya Russia na Marekani kwenye masuala ya nyuklia inazidi kupungua, makubaliano ya nyuklia ya Iran yanazidi kutiliwa shaka, matumizi ya silaha za kikemikali nchini Syria yanakiuka mwiko wa dunia kuhusu matumizi ya silaha za maangamizi.

    Katibu Mkuu amekaribisha msimamo imara ulioonyeshwa na baraza la usalama kuhusu majaribio ya nyuklia na makombora ya Korea Kaskazini. Hata hivyo ameonya kuhusu kutoaminiana kati ya Marekani na Russia, na kutishiwa kwa makubaliano ya kupunguza silaha za nyuklia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako