• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Rwanda kucheza mechi ya pili muhimu ili kufuzu robo fainali ya CHAN

    (GMT+08:00) 2018-01-19 08:58:49

    Timu ya taifa ya Rwanda (Amavubi) leo inaingia uwanjani kucheza mechi yake ya pili ya hatua ya makundi kwenye michuano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani dhidi ya Equatorial Guinea mjini Tangier.

    Rwanda yenye pointi moja kutokana na matokeo ya sare iliyopata ilipocheza dhidi ya Nigeria, inahitaji ushindi ili kujiweka katika mazingira mazuri zaidi ya kufuzu kwenda hatua ya robo fainali.

    Mechi nyingine ya kundi C itakayopigwa leo Nigeria yenye pointi moja itacheza na Libya yenye pointi tatu.

    Lakini safari ya wawakilishi wengine wa Afrika Mashariki, timu ya taifa ya Uganda itaishia hatua ya makundi kutokana na kufungwa tena katika mechi ya pili ilipocheza jana na Namibia kwa goli 1-0 mjini Marakech.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako