Uthibitisho huo umekuja baada ya kukamilika kwa ukaguzi wa mji wa Musanze ambao ndiyo haswa utakuwa maskani ya michezo hiyo mwezi Agosti.
Timu ya wakaguzi ilijumuisha wawakilishi kutoka nchi za Tanzania, Uganda, Kenya na Rwanda ikiongozwa na Rais wa FEASSA Justus Mugisha.
Rwanda ambayo inaandaa michezo hiyo kwa mara ya pili ikiwa imewahi kufanya hivyo mwaka 2015, inatarajia kupokea wanamichezo 4000 (wakiwa ni wachezaji na viongozi) kutoka nchi sita za Kenya, Burundi, Tanzania, Uganda, Sudan Kusini na Rwanda.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |