• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wadau wa michezo nchini Kenya waishukuru serikali kwa kuingilia kati tatizo lililojitokeza la udhamini

  (GMT+08:00) 2018-01-19 09:07:29

  Wadau wa michezo, wakiwemo mashabiki, wachezaji, timu mbalimbali, na vyama vya michezo nchini Kenya wameishukuru na kuipongeza serikali kwa kuamua kuunda mpango utakaosaidia kunusuru kuporomoka kwa kiwango cha michezo baada ya baadhi ya wadhamini kujitoa.

  Shukrani hizo zimetolewa baada ya Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto, juzi kutangaza kuwa serikali itatoa shilingi milioni 500 kwa ajili ya kufidia ili wachezaji, timu na timu ziendelee na mipango yake.

  Baada ya wadhamini kujitoa, vyama kadhaa viliathirika ambavyo ni chama cha soka (FKF), chama cha Raga (KRU), ndondi (BAK), klabu za Gor Mahia, AFC Leopards na Nakuru All Stars, pamoja na bondia maarufu nchini Kenya Fatuma Zarika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako