• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zimbabwe inajipanga kushirikiana tena na nchi za magharibi

    (GMT+08:00) 2018-01-19 09:22:09

    Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amesema serikali yake itatuma ujumbe katika nchi za magharibi ili kuitikia juhudi zinazofanywa na nchi za Ulaya za kurejesha ushirikiano kati ya pande hizo mbili.

    Akiwahutubia wazimbabwe wanaoishi nchini Msumbiji baada ya kufanya ziara nchini humo jumatano, rais Mnangagwa amesema nchi za magharibi zimeonesha nia ya kurejesha ushirikiano na Zimbabwe kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wajumbe wa nchi hizo wanaotumwa nchini Zimbabwe kwa ajili ya lengo hilo.

    Amesema atatuma ujumbe kwenda Uingereza kwa ajili ya kuitikia wito wao wa kurejesha ushirikiano ndani ya wiki chache, na kusisitiza kuwa Zimibabwe iko wazi kwa biashara na itarekebisha sheria ya uwekezaji ili kuzivutia uwekezaji zaidi kutoka nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako