• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mchakato wa marekebisho ya katiba Burundi waendelea vizuri kabla ya kura ya maoni

    (GMT+08:00) 2018-01-19 09:55:03

    Waziri wa mambo ya ndani wa Burundi amesema kampeni ya kufafanua marekebisho ya katiba ya Burundi kabla ya kura za maoni zitakazofanyika mwezi Mei mwaka huu, inaendelea vizuri.

    Serikali ya Burundi imesifu jinsi kampeni hiyo inavyoendelea nchini kote. Ripoti kutoka mikoani na wilayani zinaonyesha kwamba wananchi wanaelewa hatua kwa hatua mabadiliko yaliyoko kwenye rasimu ya katiba.

    Mwezi Desemba mwaka jana, tume ya uchaguzi ya taifa ya Burundi ilitangaza kuwa kura za maoni kuhusu katiba zitafanyika mwezi Mei mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako