• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UN: Wasudan Kusini 700,000 wakimbia njaa mwaka jana

    (GMT+08:00) 2018-01-19 10:05:59

    Ofisi ya uratibu wa mambo ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa OCHA imesema wasudan Kusini takriban laki 7 walikimbilia nchi jirani kutokana na mgogoro, njaa na magonjwa katika mwaka 2017.

    Ofisi hiyo imesema watu milioni 4 wamekimbia makwao, wakiwemo wakimbizi milioni 1.9 wa ndani, na zaidi ya milioni 2 waliokimbilia nchi za jirani zikiwemo Uganda, Kenya, Ethiopia, Sudan na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

    Ofisi hiyo pia imesema idadi ya wasudan Kusini walioikimbia nchi yao mwaka jana, imepungua kuliko watu laki 7.6 ya mwaka juzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako