• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasisitiza kutimiza usalama wa pamoja ni msingi wa kuzuia kuenea kwa silaha za maangmizi

    (GMT+08:00) 2018-01-19 18:12:12

    Naibu balozi wa China katika Umoja wa Mataifa Wu Haitao amesema, kutimiza usalama wa pamoja ni msingi wa kufanikisha kuzuia kuenea kwa silaha za maangamizi na swala hilo linapaswa kutatuliwa kiamani kwa njia za kisiasa na kidiplomasia.

    Akizungumza kwenye mjadala wa wazi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliofanyika jana mjini New York, balozi Wu amesisitiza kuwa China inapinga kuenea kwa silaha za maangamizi na vifaa vya kuzisafirisha, na imesaini mikataba yote ya kimataifa na kujiunga na mashirika ya kimataifa yanayohusika na kuzuia kuenea kwa silaha hizo.

    Pia amesema China imeanzisha mfumo wa kuzuia kuenea na kudhibiti mauzo ya nje ili kuhakikisha sheria na kanuni husika zinatekelezwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako