• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Filamu za Kichina zapata zaidi ya dola milioni 662 za kimarekani nchi za nje kwa mwaka jana

    (GMT+08:00) 2018-01-19 18:13:10

    Gazeti la Habari za Filamu la China limesema, filamu za Kichina zilipata dola za kimarekani milioni 662.7 katika soko la nje kwa mwaka jana, ikiwa ni asilimia 11.9 zaidi ya mwaka 2016.

    Gazeti hilo limesema, filamu ya "Wolf Worrior 2", ambayo ilivunja rekodi ya mauzo nchini China, pia iliongoza kati ya filamu karibu 100 za Kichina zilizoonyeshwa nje ya nchi kwa kupata dola za kimarekani milioni 7.6 mwaka jana.

    Sekta ya filamu ya China imezidi kuwa na uhai kutokana na makubaliano 20 ya ushirikiano wa mambo ya filamu yaliosainiwa na nchi kadhaa zikiwemo India, Russia, na Hispania mwaka jana. Wakati huohuo, karibu matamasha 50 ya filamu ya kimataifa yanayoonyesha filamu za Kichina yameongeza kasi ya mabadilishano ya kiutamaduni na nchi nyingine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako