• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Syria yasema uwepo wa kijeshi wa Marekani nchini humo ni haramu

    (GMT+08:00) 2018-01-19 18:24:28

    Wizara ya mambo ya nje ya Syria imesema, uwepo wa jeshi la Marekani nchini humo ni haramu na ujenzi mpya wa Syria haukaribishi ushiriki wa Marekani.

    Taarifa ya wizara hiyo imekuja baada ya hivi karibuni, Marekani kusema itaendelea kudumisha uwepo wa jeshi lake nchini Syria. Wizara hiyo imesema, uwepo wa jeshi la Marekani nchini Syria umekiuka sheria ya kimataifa, na ni kitendo cha kuingilia mamlaka ya nchi nyingine. Taarifa hiyo pia imesema, lengo la Marekani sio kuangamiza kundi la IS, bali ni kutoa ulinzi kwa kundi hilo ambalo Syria inadai kuwa inaliunga mkono.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako