• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yatoa masharti kwa viwanda vya Sukari nchini humo

    (GMT+08:00) 2018-01-19 19:00:13

    Serikali ya Tanzania imetoa masharti ili kuruhusu kuchukuliwa kwa sukari ya viwandani iliyokwama katika Bandari ya Dar es Salaam ili kuviwezesha viwanda vitano vilivyoagiza visifungwe kwa kukosa malighafi .

    Hatua hiyo imefikiwa baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kuishauri serikali kuruhusu sukari hiyo iliyokuwa inashikiliwa na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), kuchukuliwa ili kuviokoa viwanda hivyo. Viwanda vilivyolalamika sukari yao kuzuiwa na TRA bandarini ni Kiwanda cha Sayona cha Dar es Salaam na Mwanza, Kiwanda cha Ivory cha Iringa, Kiwanda cha Iringa Food Beverage cha Iringa na Kiwanda cha Anjari cha Tanga.

    Aidha kiwanda cha Coca-Cola Kwanza Limited cha Dar es Salaam kililalamika kwa Kamati hiyo ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, kutotosha kwa sukari waliyoagiza kutokana na kibali kipya walichopewa na hivyo nao kuwa katika tishio la kufunga kiwanda.

    Uamuzi wa kupewa masharti ya mikataba kwa viwanda hivyo, ulifikiwa mjini Dar es salaam katika kikao kilichowajumuisha Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Sadick Murad, Mnadhimu wa Shughuli za Serikali bungeni ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Bunge, Jenista Mhagama na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako