• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya kupanua taasisi ya TTI ili kukuza sekta ya viwanda

    (GMT+08:00) 2018-01-19 19:09:07

    Serikali ya Kenya inapanga kupanua taasisi ya mafunzo ya ngozi na nguo TTI kwa lengo la kusajili wanafunzi zaidi katika muda wa miezi kadhaa ijayo kwa lengo la kukuza sekta ya viwanda nchini Kenya.Waziri wa leba na utangamano katika jumuiya ya Afrika mashariki Bi Phylis Kandie amesema hatua hiyo ilikuwa kwa lengo la kukuza uwezo wa taasisi hiyo kutoa mafunzo kwa maelfu ya vijana ambao hawajajiunga na vyuo vikuu na wasio na kazi. Kandie amesema lengo haswa ni kukuza sekta ya ngozi na nguo kupitia utoaji wa mafunzo.Wakati huohuo waziri wa viwanda, biashara na vyama vya ushirika wa Kenya Bw Adan Mohammed wanalenga kurekebisha wajibu wa mamlaka ya kitafifa ya utoaji mafunzo ya viwanda kwa lengo la kupanua uwezo wake wa utoaji mafunzo. Kwa sasa taasisi hiyo hutoa mafunzo kwa wanafunzi 40,000 hadi elfu 50 kwa mwaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako