• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • M-KOPA SOLAR kuunda nafasi zaidi za ajira

    (GMT+08:00) 2018-01-19 19:09:26

    Kampuni ya M-kopa Solar inalenga kubuni nafasi zaidi za ajira kwa kutumia vidubwasha vya kuvuta miale ya jua vinavyoundiwa nchini Kenya. Hadi kufikia sasa taasisi hiyo imeuza jumla ya vidudubwasha laki 1 vilivyotengenezwa nchini Kenya na kampuni ya Solinc iliyopo Naivasha katika kaunti ya Nakuru.Mwenyekiti wa Kampuni hiyo Mugo Kebati ameongeza kuwa wanalenga kununua vidudubwasha laki 5 katika muda wa miaka 2 ijayo vilivyoundwa nchini Kenya.Amesema utumizi wa miale ya jua umesaidia kuwajumuisha hata wale wenye mapato ya chini katika uendelezaji wa uchumi. Meneja mkuu wa Solinc Bw Haijo Kuper ameeleza kuwa ushirikiano wake na M-KOPA umechangia kuajiriwa kwa watu 50 wanaohusika moja kwa moja na bidhaa hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako