• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mashindano ya Baiskeli, Joseph Areruya wa Rwanda ashinda mbio za Dunia

  (GMT+08:00) 2018-01-22 09:33:59

  Joseph Areruya wa Rwanda, ameibuka bingwa wa mashindano ya kimataifa ya baiskeli ya Gabon baada ya kutumia saa 23 dakika 52 na sekunde 24 za mbio hizo zenye urefu wa kilomita 967.5 zilizomalizika jana mjini Libreville.

  Kwa ushindi huo, Areruya anaweka rekodi ya pekee kwa kushinda mataji makubwa mfululizo pekee yake bada ya kushinda kwenye ubingwa wa Afrika kupitia mashindano ya Tour Du Rwanda.

  Mshindi wa pili katika mashindano ya Gabon, alikuwa Holler Nikodemus kutoka Ujerumani anayeitumikia timu ya Bike Aid, na nafasi ya tatu ikienda kwa Guadin Damien wa Ufaransa.

  Na katika kipindi cha miaka kumi iliyopta Areruya anakuwa mwendeshaji baiskeli wa tatu kutoka Afrika kuwahi kutwaa ubingwa huo, baada ya Rafaa Chtiioui wa Tunisia kushinda mwaka 2015, na Natnael Berhane kushinda mwaka 2014, lakini miaka mining yote ubingw ukienda Ulaya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako