• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katika ligi kuu Hispania Ronaldo, Messi, Bale na Messi wafunga magoli mawili kila mmoja

    (GMT+08:00) 2018-01-22 09:36:08
    Wachezaji Lionel Messi na Luis Suarez wameng'ara vilivyo wakati timu yao ya Barcelona ilipoifunga Real Betis kwa magoli 5-0 na kufikisha pointi 54 kileleni mwa msimamo ikiwa ni 11 zaidi ya timu iliyoko nafasi ya pili.

    Suarez alifunga magoli mawili katika dakika ya 69 na 89, na mwenzake Lionel Messi akifunga kunako dakika ya 64 na 80, lakini goli la tano la wakatalan hao lilifungwa na kiungo Ivan Rakitic wa Croatia.

    Mahasimu wa Barcelona, Real Madrid nao jana wamefanikiwa kupata ushindi mnono wa magoli 7-1 walipocheza dhidi ya Deportivo la Coruna.

    Katika mechi hiyo, Cristiano Ronaldo, Gareth Bale na Nacho Monreal walifunga magoli mawili kila mmoja, na goli moja likifungwa na kiungo wa Croatia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako