• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuhimiza maendeleo ya magari yanayotumia nishati mpya

    (GMT+08:00) 2018-01-22 17:35:12

    Kongamano la mwaka 2018 kuhusu maendeleo ya magari ya umeme nchini China limefanyika hivi leo hapa Beijing. Waziri wa sayansi na teknolojia wa China Bw. Wan Gang kwenye kongamano hilo amesema, China itahimiza maendeleo ya hali ya juu ya magari yanayotumia nishati mpya, kwa mujibu wa mwelekeo wa kuwa ya umeme na ya teknolojia za kisasa, na kutilia maanani zaidi uvumbuzi wa sekta, teknolojia na sera.

    Kongamano hilo la siku mbili lenye kauli mbiu ya "kufuata mwelekeo wa mageuzi ya dunia, na kutimiza maendeleo ya hali ya juu", limewavutia wajumbe zaidi ya elfu moja kutoka nchini China na nchi za nje. Waziri wa sayansi na teknolojia wa China Bw. Wan Gang amesema hadi sasa China imejenga mtandao wa kutengeneza vipuri na magari mazima yanayotumia nishati mpya, na kupiga hatua kubwa katika utafiti na uvumbuzi wa vipuri muhimu na kuvitengeneza kwa lengo la kibiashara, na pia China imekamilisha mfumo endelevu wa sera za kuunga mkono maendeleo ya magari hayo kwa pande zote na kwa muda mrefu. Anasema,

    "Mwaka 2017, idadi ya mauzo ya magari yanayotumia nishati mpya katika nchi kubwa duniani ilizidi milioni 1.42, huku idadi hiyo nchini China ikiwa laki 7.77, idadi ambayo inatarajiwa kuongezeka na kuwa milioni moja kwa mwaka huu."

    Hata hivyo maendeleo ya magari yanayotumia nishati mpya bado yanakabiliwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo kuwa na betri dhaifu, upungufu wa vibanda vya kuchaji betri, ukosefu wa mfumo kamili wa huduma na uungaji wa kutosha za sera kutoka serikali.

    Bw. Wan amesema katika siku za baadaye, China itahimiza maendeleo ya hali ya juu ya magari yanayotumia nishati mpya, kwa mujibu wa mwelekeo wa kuwa ya umeme na ya teknolojia za kisasa, na kutilia maanani zaidi uvumbuzi wa sekta, teknolojia na sera. Anasema,

    "Katika upande wa kodi, wakati tunapomaliza ruzuku kwa mashirika ya kutengeneza magari yanayotumia nishati mpya, tutarefusha muda wa kutoa ruzuku kwa wateja wa magari hayo. Aidha, tutaharakisha kuanza mfumo wa kutunza matumizi ya magari hayo, pamoja na sera za biashara ya hewa ya Carbon."

    Mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya BYD ambayo ni kampuni kubwa zaidi la kutengeneza magari yanayotumia nishati mpya nchini China Bw. Wang Chuanfu, anakadiria kuwa hadi kufikia mwaka 2020, China itakuwa na uwezo wa kuzalisha magari yanayotumia nishati mpya milioni mbili kwa mwaka.

    Mkurugenzi mtendaji wa kamati ya mabingwa mia moja wanaoshughulikia magari ya umeme Bw. Chen Taiqing anaona kuwa, katika siku za baadaye, magari ya aina mpya yatakuwa vitu vya kimsingi katika miji ya kisasa. Amependekeza kuwa serikali inapaswa kutunga mpango ili kuelekeza matarajio ya jamii na soko. Anasema,

    "Inakadiriwa kuwa hadi kufikia mwaka 2030, idadi ya mauzo ya magari ya umeme nchini China itazidi milioni 15. Hali ambayo italazimisha serikali kutoa mpango mahsusi, ili kusukuma mbele mageuzi ya pande mbalimbali."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako