• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda:Mikopo ya juu ya athiri sekta ya mauzo ya nje

    (GMT+08:00) 2018-01-22 19:33:20
    Mkopo wa gharama kubwa ni mojawapo ya matatizo wafanyibishara wa mauzo ya nje wametambua ambayo inawazuia kuinua sekta hiyo ili kuwezesha nchi kukataa ada kubwa wanazo tumia katika kuagiza.

    baadhi ya benki za biashara zimepunguza viwango vya mikopo yao hadi asilimia 17,lakini bado wauzaji wanasema bado ni iko juu sana kwao.

    Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa pili wa mauzo ya kila mwaka huko Kampala Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya Kukuza mauzo ya Nje ya Uganda (UEPB), Elly Twineyo Kamugisha, amesema wanahitaji mikopo ya bei nafuu kwa sababu mabenki ya kibiashara ni ghali sana.

    Takwimu za hivi karibuni kutoka Benki ya Uganda za mnamo mwezi Novemba 2017, inaonyesha uganda ilifanya mauzo ya nje na huduma (rasmi na isiyo rasmi) yenye thamani ya shilingi trilioni 11.5, kutoka Sh trilioni 9.8 iliyosajiliwa mwaka uliopita.

    Hiyo ni ongezeko la Sh trilioni 1.7 lakini utendaji huu unafunikwa bili kubwa za uagizaji za sh trilioni 20.8.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako