• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa 30 wa Umoja wa Afrika waanza

  (GMT+08:00) 2018-01-22 19:43:42

  Kikao cha kawaida cha 35 cha Kamati ya Kudumu ya Wawakilishi wa Umoja wa Afrika kimefunguliwa rasmi leo katika makao makuu ya umoja huo mjini Addis Ababa, Ethiopia.

  Mkutano huo umewakutanisha pamoja mabalozi wa nchi 55 wanachama na maofisa muhimu wa umoja huo walioko mjini Addis Ababa. Chini ya kaulimbiu ya "Kushinda Vita Dhidi ya Rushwa: Kudumisha Mwelekeo wa Mageuzi ya Afrika", Kamati hiyo itapokea na kujadili masuala yanayohusiana na kilimo, uchukuzi, sayansi na teknolojia, teknolojia ya habari na mawasiliano, na masuala mengine yanayohusiana na mambo ya kisheria na kifedha.

  Akifungua mkutano huo, mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat amesisitiza tena kuwa nchi wanachama wa umoja huo zinapaswa kuchukua nafasi kubwa katika kupambana na rushwa, jambo linalotiliwa maanani na shirika hilo la kikanda kwa mwaka huu na kuendelea. Pia mwenyekiti huyo amesisitiza umuhimu wa mageuzi ya Umoja wa Afrika yenye lengo la kuongeza ufanisi wa utendaji.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako