• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rwanda kucheza na Libya leo

  (GMT+08:00) 2018-01-23 09:23:55

  Leo ni leo nchini Morocco ambako wawakilishi pekee waliosalia katika mashindano ya ubingwa wa mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani, Rwanda watacheza mechi muhimu kwa ajili ya kufuzu hatua ya robo fainali.

  Rwanda watashuka dimbani leo mjini Tangier kucheza na mabingwa watetezi wa michuano hiyo, Libya katika mechi yao ya mwisho kwenye hatua ya makundi.

  Ushindi ni lazima kwa Rwanda ili kusonga mbele, licha ya kuwa sare itawafaa endapo Nigeria wataifunga Equatorial Guinea katika mechi nyingine ya kundi C itakayopigwa muda huo huo mjini Agadir.

  Kocha mkuu wa Rwanda Antoine Hey ameweka wazi kuwa mchezo huo, hautakuwa mrahisi isipokuwa watapambana ili kufuzu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako