• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Utata wazuka baada ya Marais wawili kuchaguliwa kwa ajili ya kuongoza chama cha ngumi cha taifa

    (GMT+08:00) 2018-01-23 09:25:01
    Utata umeendelea kuibuka juu ya maendeleo ya mchezo wa masumbwi nchini Uganda, baada ya kufanyika chaguzi kuu mbili za Shirikisho la ngumi nchini Uganda UBF, lakini kila moja ikitoa viongozi wake, na kuifanya UBF iwe na marais wawili.

    Upande mmoja, umemchagua Moses Muhangi kuwa Rais wake, na uchaguzi huo ulishuhudiwa na mwakilishi wa Umoja wa vyama vya masumbwi duniani AIBA, lakini upande wa pili rais anayemaliza muda wake Kenneth Gimungu ametetea kiti chake katika uchaguzi ulioshuhudiwa na kamati ya Olimpiki ya Uganda.

    Lakini baraza la michezo nchini Uganda halijafika kushuhudia uchaguzi wa upande wowote katika mchakato huo.

    Kuhusu, mapingamizi yaliyopelekwa mahakamani, Januari 19, Jaji Lydia Mugambe alitoa uamuzi kuwa shirikisho hilo lifanye mambo yake bila kuvunja sheria za nchi na hata kama kuna pande zinahasimiana, haki itendeke kwa wanachama wote washiriki kila jambo linalowahusu isipokuwa wale amabao hawatathibitishwa na bodi ya wadhamini wa shirikisho hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako