• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mchezaji wa Tanzania ashikiliwa na Polisi

    (GMT+08:00) 2018-01-23 09:25:48
    Beki wa Kagera Sugar Juma Nyoso anashikiliwa na jeshi la polisi mijini bukoba kwa tuhuma za kumshambulia kwa kumpiga shabiki mmoja baada ya mchezo wa ligi kuu Tanzania bara kati ya Kagera Sugar dhidi ya Simba uliomalizika kwaSimba kushinda 2-0 kwenye uwanja wa Kaitaba.

    Inasadikiwa kuwa, shabiki aliyepigwa na nyoso ni wa Kagera Sugar, tukio hilo lilitokea baada ya mchezo huo kumalizika ambapo wakati wachezaji wa Kagera Sugar wakielekea kwenye vyumba vya kubadilishia nyuo, inaelezwa baadhi ya mashabiki wa timu hiyo walikuwa wakiwatolea maneno makali wachezaji wao kiasi kwamba Nyoso alishindwa kuzuia harisa zake na kumpiga mmoja wa mashabiki hao ambaye alizimia papo hapo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako