• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Liverpool yafungwa kwa mara ya kwanza

    (GMT+08:00) 2018-01-23 09:28:10
    Rekodi ya kutofungwa katika mechi nyingi iliyokuwa imeanza kuandikwa na klabu ya Liverpool imefutwa jana ilipofungwa goli 1-0 na Swansea City.

    Goli la Swansea lilifungwa na Alfie Mawson katika dakika ya 40 ya mchezo huo, na Liverpool ilikuwa haijafungwa katika mechi 18 tangu mara ya mwisho mwezi Oktoba mwaka jana ilipokubali kipigo cha magoli 4-1 kutoka kwa Tottenham.

    Katika mechi sita ilizocheza tangu imwajiri kocha mpya Carlos, huu ni ushindi wa kwanza, imepoteza mara moja na imetoa sare mara nne, hivyo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika safari yake ya kujinusuru kushuka daraja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako