• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: VW kuanza kutengenezwa Rwanda Mei

    (GMT+08:00) 2018-01-23 19:17:22
    Gari la kwanza lililotengenezwa nchini Rwanda, linatarajiwa kuwa barabarani Mei mwaka huu.

    Kampuni ya kutengeneza magari ya Volkswagen (VW) ya Ujerumani, ipo kwenye maandalizi ya kutengeneza aina tatu za magari nchini humo.

    VW imetangaza kuwekeza Dola za Marekani milioni 20 (takribani Faranga bilioni 17 za Rwanda) kwenye uanzishaji kiwanda cha kutengeneza magari nchini humo. Uongozi wa kampuni hiyo umesema sehemu kubwa ya fedha hizo, zitatumika kutengeneza magari na kuanzisha maeneo ya uunganishaji magari.

    Kampuni hiyo tayari imesajili kampuni nchini humo iitwayo, Volkswagen Mobility Solutions Rwanda.

    Ofisa Mtendaji Mkuu wa VW nchini Afrika Kusini, Thomas Schafer alisema, wamechagua kuwekeza Rwanda kwa kuwa kuna mazingira mazuri ya kufanya biashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako