• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Mafunzo ya ufundi kupitia  simu za mkononi yafaa wanafunzi Tanzania

    (GMT+08:00) 2018-01-23 19:17:43
    Mpango wa kutoa mafunzo ya ufundi kupitia aplikesheni ya simu za mkononi unaoendeshwana kampuni ya Airtel kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mafunzo ya ufundi Stadi (VETA), umewavutia takribani wanafunzi 10,000.

    Wanafunzi hao tayari wamejiandikisha kwa ajili ya masomo ya ufundi stadi kupitia aplikesheni ya VSOMO.

    Chini ya utaratibu huo, wanafunzi hao wataweza kusoma kozi mbalimbali za ufundi.

    Kaimu Mkuu wa chuo cha ufundi cha VETA kituo cha Kipawa, Harold Mganga amesema kuwa mafunzo ya ufundi ya muda mfupi yamekuwa yakitolewa na katika vyuo cha VETA kwa miaka mingi.

    Mpaka sasa wanafunzi 9,975 wamejiandikisha kupata mafunzo hayo na zaidi ya watu 33,000 wameshapakuwa aplikesheni hiyo ya VSOMO kupitia simu zao za mkononi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako