• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Kenya yapanga kupunguza matumizi ya serikali

    (GMT+08:00) 2018-01-23 19:18:05
    Serikali ya Kenya inapanga kupunguza matumizi yake ndani ya miaka mitano ijayo, ili kukata bajeti ifikie viwangi vinavyokubalika kimataifa.

    Mwanya kwenye bajeti ya kitaifa ulifikia asilimia 8.9 kwenye mwaka uliopita wa kifedha na waziri wa fedha nchini humo Henry Rotich anasema sasa wanalenga kupunguza mwanya huo hadi asilimia 6.

    Wataalam na mashirika ya kifedha duniani yamekuwa yakiomba Kenya kupunguza madeni yake na pia mikopo ya kufadhili miradi mikubwa.

    Serikali ya Uhuru Kenyatta tangu mwaka 2013 imekuwa ikikopa fedha nyingi, lakini pia bila mikopo hiyo haingeweza kutekeleza miradi yake kama ule wa reli ya kisasa na miradi ya kawi na barabara.

    Deni la kitaifa lilifikia shilingi trilioni 4.8 septemba mwaka jana likiwa limeongezeka kutoka trilioni 3.5 machi 2015.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako