• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Zhang Dejiang akutana na spika wa bunge la Kiarabu

  (GMT+08:00) 2018-01-23 20:00:44

  Spika wa bunge la umma la China Bw. Zhang Dejiang leo hapa Beijing amekutana na spika wa bunge la Nchi za Kiarabu Bw. Meshal Faham M. Al-Sulami.

  Katika mazungumzo yao, Bw. Zhang Dejiang amesema, ziara hiyo ni mara ya kwanza ya mawasiliano rasmi kati ya pande hizo mbili, na ina umuhimu mkubwa kwa kuzidisha uhusiano kati ya China na nchi za kiarabu. Amesema China inapenda kushirikiana na nchi za kiarabu, kuhimiza urafiki wa jadi kati ya pande hizo mbili kupata matokeo makubwa zaidi.

  Bw. Sulami amesema, bunge la Nchi za Kiarabu linapenda kuimarisha mawasiliano ya kirafiki kati yake na bunge la umma la China, na kuhimiza maendeleo zaidi ya ushirikiano katika siasa, uchumi, utamaduni na sekta nyingine.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako