• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • timu ya taifa ya Rwanda yapokelewa kishujaa mjini Kigali

  (GMT+08:00) 2018-01-24 09:49:16

  Jana ilikuwa shangwe mjini Kigali, baada ya mashabiki kujitokeza kwa wingi kuwalaki kishujaa washindi wa mashindano ya dunia ya baiskeli yaliyomalizika jumapili iliyopita mjini Libreville nchini Gabon.

  Timu hiyo ya Rwanda ikiongozwa na bingwa Joseph Areruya iliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kigali majira ya jioni, na kisha kuelekea uwanja wa Amahoro kwa ajili ya hafla maalum ya kuwapongeza.

  Wakati wa safari ya kutoka uwanja wa ndege wa Kigali kwenda Uwanjani maelfu ya mashabiki walijipanga barabarani kwa ajili ya kuwashangilia.

  Waendesha baiskeli walioipeperusha vyema bendera ya Rwanda ni Valens Ndayisenga, Jean Damascene, Didier Munyaneza, Bonaventure Uwizeyimana na Paul Ukiniwabo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako