• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda yashindwa kufuzu robo fainali ya mashindano ya Afrika

    (GMT+08:00) 2018-01-24 09:49:42
    Timu ya taifa ya Rwanda imeyaaga mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN, mara baada ya kukubali kipigo cha goli moja 1-0 katika mechi yao mwisho ya hatua ya makundi.

    Rwanda walifungwa na mabingwa watetezi wa michuano hiyo Libya, ambapo sasa wanashika nafasi ya tatu katika kundi C.

    Rwanda ambayo ilikuwa timu pekee kutoka Afrika Mashariki iliyokuwa imesalia katika mashindano hayo, ilifanikiwa kuumiliki mpira katika mechi hiyo katika dakika zote, kabla ya goli la maajabu la Libya lililopatikana katika dakika ya 93 kupitia Emultasem Abushnaf.

    Kutokana na mateoke ya jana, Libya inaungana na Nigeria kufuzu, na zinasubiri mshindi wa kwanza na mshindi wa pili kutoka kundi D watakaojulikana baada ya mechi zitakazopigwa leo, katika Congo na Angola, lakini pia Burkina Faso dhidi ya Cameroun.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako