• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kombe la Ligi Uingereza: Manchester City yafuzu fainali

    (GMT+08:00) 2018-01-24 09:50:23
    Manchester City jana imefuzu fainali ya mochuano ya kombe la ligi nchini Uingereza baada ya kuifunga kwa magoli 3-2 Bristol City katika mechi ya marudiano ya nusu fainali.

    Ushindi huo unaifanya City isonge mbele kwa jumla ya magoli 5-3 kufuatia ushindi wa kwanza wa magoli 2-1 iliopata wiki mbili zilizopita.

    Kwa kocha Pep Guradiola, ushindi huu uliandika historia kwa kuwa ulikuwa ni ushindi wa 363 katika mechi 500 alizofikisha jana tangu aanze kazi ya ukufunzi wa soka.

    Timu hiyo sasa inasubiri mshindi wa mechi nyingine ya nusu fainali itakayopigwa leo mjini London kati ya Arsenal na Chelsea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako