• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ligi ya NBA Marekani: Houston yaishinda Miami

    (GMT+08:00) 2018-01-24 09:51:20
    Timu ya Houston Rockets ikiogozwa na nyota wake James Harden jana imefanikiwa kuifunga, timu ya Miami Heat kwa pointi 99-90, zilizofanya timu hiyo ijitengenezee mazingira mazuri ya kufuzu nusu fainali ya ligi hiyo ngazi ya kanda.

    Licha ya jitihada za nyota wa kimataifa Hassan Whiteside aliyefunga pointi 22 peke yake, na kuifanya timu hiyo iongoze kwenye robo ya kwanza ya mchezo huo, Miami haikuweza kujinusuru na ushindi mwembamba wa Houston ambayo ilinufaika na kazi nzuri ya James Harden aliyefunga 28 peke yake.

    Asubuhi hii kwa majira ya Afrika mashariki kunafanyika mechi nyingine kubwa za NBA mabingwa wa mwaka 2014, San Antonio Spurs wanacheza na mabingwa wa mwaka 2016 Cleveland Cavaliers, lakini Golden State Warriors wako ugenini kucheza na New York Knicks.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako