• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AIIB yapata mafanikio makubwa katika kuboresha miundo mbinu duniani

    (GMT+08:00) 2018-01-24 19:00:50

    Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu ya Asia AIIB ilianzishwa tarehe 16, Januari mwaka 2016. Katika miaka miwili iliyopita, idadi ya wanachama wake imeongezeka kuwa 84 kutoka 57 ya awali. Hadi sasa benki hiyo imewekeza miradi 24 ya miundombinu katika nchi 12.

    Mwezi Desemba mwaka jana, bodi ya wakurugenzi ya AIIB ilitangaza kupitisha ombi la kujishirikisha la Visiwa vya Cook, Vanuatu, Belarus na Ecuador, na idadi ya wanachama wa benki hiyo iliongezeka kuwa 84. Hii ilikuwa mara ya nne ya benki hiyo kuongeza wanachama wake. Mtafiti wa taasisi ya utafiti wa uhusiano wa kimataifa ya China Bi Chen Fengying anasema,

    "Zina madhumuni tofauti kwa kujiunga na AIIB, nafikiri sababu kuu ni fursa. Uwekezaji kwa miundombinu unahitajika katika sehemu zote duniani haswa barani Asia. Pamoja na pendekezo la China la "Ukanda Mmoja na Njia Moja", AIIB inaweza kutoa mchango mkubwa zaidi kwa ajili ya maendeleo ya nchi mbalimbali duniani."

    Katika miaka miwili iliyopita, miradi iliyofuatiliwa na AIIB yote ni kuhusu miundombinu. Tarehe 11, Desemba mwaka jana, benki hiyo ilitangaza mradi wake wa kwanza nchini China ulizinduliwa mjini Beijing, na kutoa mkopo wa dola milioni 250 za kimarekani kwa ajili ya ujenzi wa mabomba ya kusafirisha gesi, ili kupunguza uchafuzi wa hewa. Wakati huo huo, miradi ya treni za kupita chini ya ardhi nchini India na mtandao wa kasi wa Internet nchini Amman ilipitishwa.

    Takwimu zinaonesha kuwa, katika miaka miwili iliyopita, AIIB imefanya miradi 24 ya miundombinu katika nchi 12, kwa kutoa mikopo zaidi ya dola bilioni 4.2 za kimarekani. Miradi hiyo ni pamoja na ukarabati wa nyumba duni, kingo dhidi ya mafuriko, mabomba ya gesi, barabara za kasi kubwa, barabara vijijini, mtandao wa kasi wa Internet, utoaji wa umeme. Bi Chen Fengying amesisitiza kuwa, mikopo ya dola bilioni 4.2 ya AIIB ilileta uwekezaji mwingine zaidi ya bilioni 20 kutoka serikali na mashirika ya kibinafsi. Anasema,

    "AIIB imetumia vizuri uzoefu wa mashirika mengine ya kifedha duniani. ingawa mikopo iliyotolewa nayo ni dola bilioni 4.2 tu, lakini ilileta uwekezaji mwingine zaidi ya bilioni 20. Benki ya Dunia pia inafanya hivyo, lakini AIIB imefanya vizuri zaidi."

    Mwaka jana AIIB ilipata tathmini ya ngazi ya 3A kutoka mashirika matatu makuu duniani ya Moody's, Standard & Poor's na FITCH. Hali ambayo imeongeza imani ya wawekezaji wa kimataifa kuhusu uwezo wa benki hiyo kaitika kuongoza shughuli za uwekezaji duniani na kuchangia maendeleo ya kimataifa. Bi Chen Fengying anasema,

    "AIIB ni benki yenye ufanisi mkubwa na isiyo na ufisadi wowote. Shughuli zake ni wazi. Hii ni sababu ya mashirika matatu makuu ya kimataifa kuipa tathmini ya ngazi ya juu. Ubora wa benki hiyo umetambuliwa kutokana na juhudi zake za miaka miwili iliyopita."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako