• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya kujenga eneo la biashara huru mjini Mombasa

    (GMT+08:00) 2018-01-24 19:20:33
    Mji wa Mombasa unatarajiwa kuwa na eneo la biashara huru kwa ajili ya magari mwaka huu .

    Hatua hii inalenga kutoa maelfu ya ajira kwa wafanyabiashara na watoaji huduma.

    Eneo la biashara huru kama vile Dubai,ni lango usafirishaji upya ambapo bidhaa zinazopitia hapo na kuelekea sehemu nyengine huhifadhiwa kwa muda ili kuepuka vikwazo vya forodha na taratibu ndefu ambazo bidhaa za nyumbani hupitia.

    Ujenzi wa kituo hicho nchini Kenya ,takriban miaka minne tangu baraza la mawaziri kupitisha mpango huo,unamaanisha kuwa uagizaji wa magari yanayoelekea katika masoko mengine katika kanda utapokelewa mwanzo na kuainishwa Mombasa.

    Bidhaa hizo zitalipiwa ushuru pindi zitakapofika sehemu zilikoagizwa.Nchi itanufaika kwa fursa za ajira kwa wananchi wake na ukusanyaji wa malipo ya mizigo.

    Katika rasimu ya taarifa ya bajeti iliyotolewa ijumaa iliyopita,Waziri wa Fedha Henry Rotich anakadiria kuwa kituo hichoi cha Mombasa kwenye ardhi ya ekari 1,000 kitashughulikia magari 100,000 kwa mwaka.

    Kituo hicho cha eneo la biashara huru (FTZ) kinajengwa ili kushughulikia nchi zisizo na bahari chini ya Soko la Pamoja kwa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako