Bandari ya Mombasa haina kituo cha kusambaza umeme katika eneo la meli kutia nanga bandarini na kusababisha meli kuacha injini zikinguruma na kutoa moshi mwingi.
Mkuu wa kituo cha Maritime Technology Cooperation Centre (MTCC) Africa,mhandisi Michael Muchiri amesema ujenzi wa kituo hicho utagharimu Sh150 milioni.
Muchiri amesema ujenzi wa kituo cha kusambaza umeme katika meli zinazoleta mizigo bandarini ni muhimu kwa kuwa kitawezesha kupunguza kiwango cha moshi unaotoka katika meli ambao hudhuru mazingira ya bahari.
Ujenzi huo wa kituo hicho utawezesha bandari kusambaza umeme kwa meli za mizigo kuzima injini ili kukabili athari za moshi wenye gesi ambazo hudhuru mazingira ya bahari.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |