• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda imeandikisha ongezeko la uuzaji nje bidhaa za viwandani.

    (GMT+08:00) 2018-01-24 19:21:27
    Hivi sasa Uganda inasafirisha bidhaa za viwandani katika kanda ya Afrika Mashariki zenye thamani ya $1 bilioni (Shs3.6 trillion) kutoka $10 milioni (Shs36.5 billion) ambazo nchi hiyo ilipata miaka 10 iliyopita.

    Akizungumza wakati wa kongamano la wauzaji bidhaa la kila mwaka jijini Kmapala jana,Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Uimarishaji wa mauzo ya nje ya Uganda Bw Elly Twineyo alisema mwenendo huo unaoyesha kuwa Uganda inabadilika kutoka mauzo ya bidhaa za kilimo.

    Alisema ubora wa bidhaa zao za viwandani umeimarika pakubwa na kutokana na kuongezeka kwa uwezekaji katika ongezeko la thamani, usafirishaji wa bidhaa za viwandani umeongezeka.

    Wataalamu wanasema hali hii imetokana na kuongezeka kwa idadi ya watu katika kanda,na vilevile mapato.

    Bidhaa zinazonunuliwa kwa wingi kutoka Uganda ni bidhaa za ujenzi kama vile sementi,mabati na vyuma.

    Bidhaa hizi mara nyingi huuzwa magharibi mwa Kenya,Sudan kusini,Burundi na Rwanda,DR Congo pamoja na baadhi ya nchi katika ukanda wa Comesa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako