• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Timu ya taifa ya Masumbwi yazuiwa kwenda kushiriki mashindano ya jumuiya ya dola Australia

  (GMT+08:00) 2018-01-25 09:24:37

  Timu ya taifa ya masumbwi ya Rwanda haitakwenda kushiriki mashindano ya jumuiya ya madola yatakayofanyika Aprili 4 hadi 15 mwaka huu nchini Australia.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyothibitishwa na Rais wa kamati ya kitaifa ya Olimpiki Valens Munyabagisha, chama cha ngumi hakikukidhi vigezo vilivyowekwa kwa ajili ya kwenda kushiriki, na kigezo kimojawapo ikiwa ni kuandaa mashindano ya kitaifa jambo ambalo halikufanyika.

  Akizitaja timu zitakazoshiriki Rais huyo amesema ni Riadha, Waendesha baiskeli, mpira wa wavu kwa viwanja vya ufukweni na timu ya wanamichezo wa kunyanyua vitu vizito.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako