• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Daktari wa timu ya Olimpiki ya Marekani afungwa miaka 175 jela kufuatia udhalilishaji wa wanawake kingono

    (GMT+08:00) 2018-01-25 09:25:12

    Daktari maarufu wa timu ya Olimpiki ya Marekani Larry Nassar amefungwa miaka 175 baada ya wanawake 160 kati ya zaidi ya 200 aliowadhalilisha kijinsia kwa nyakati tofauti kutoa ushahidi mahakamani.

    Nassar alikiri kutenda makosa kumi yaliyotolewa ushahidi jana mahakamani, dhidi ya wasichana na wanawake waliokuwa timu za olimpiki.

    Jaji Rosemarie Aquilina alitupilia mbali ombi la Nasser la kusamehewa kwani tayari alikwishaanza kutumikia kifungo cha miaka 60 kutokana na hatia ya kumiliki filamu za ngono za watoto.

    Kwa kuhitimisha Jaji huyo alimwambia Nasser hafai kutoka kifungoni na akisema kwa kumsaidia atasaini hati ya kifo chake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako