• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Cape Town City yaeleza kufurahishwa na usajili wa mchezaji Katerrega wa Uganda

    (GMT+08:00) 2018-01-25 09:26:36
    Kocha mkuu wa Timu ya Cape Town City inayoshiriki ligi kuu ya nchini Afrika Kusini Benni McCathy, ameeleza matumaini makubwa ya kufanya vizuri kwenye mechi za kitaifa na kimataifa baada ya kuongeza nguvu kwa kumsajili winga wa kushoto wa kimataifa wa Uganda Allan Katerrega.

    Katerrega mwenye miaka 23 anajiunga na City akitokea klabu ya KCCA aliyokuwa akiitumikia kwa mkopo akitokea AFC Leopards ya Kenya, lakini akiwahi kuzichezea timu za Victoria University na Tusker FC.

    Cape Town City ipo katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Afrika Kusini nyuma ya vinara Mamelodi Sundowns baada ya kucheza mechi 18.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako