• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • kombe la ligi Uingereza; Arsenal yaifunga Chelsea na kufuzu fainali

    (GMT+08:00) 2018-01-25 09:27:28
    Arsenal imefanikiwa kuweka hai matumaini ya kutwaa ubingwa wa michuano ya kombe la ligi la nchini uingereza baada ya kufuzu fainali msimu huu.

    The gunners jana waliwafunga Chelsea kwa magoli 2-1 kwenye mechi ya pili ya nusu fainali iliyopigwa mjini London.

    Chelsea walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia Eden Hazard kunako dakika ya saba, lakini sherehe hiyo haikudumu kwani dakika tano baadaye Arsenal walisawazisha kupitia goli la kujifunga baada ya Nacho Monreal kupiga shuti kulilenga lango Chelsea.

    Goli la pili la Arsenal lilipatikana katika dakika ya 60 kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara waliyoyafanya dhidi ya Chelsea, hivyo timu hiyo imekata tiketi ya kucheza fainali dhidi ya Manchester City itakayopigwa February 25.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako