• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yahimiza kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja duniani

  (GMT+08:00) 2018-01-25 17:28:47

  Mkutano wa 48 wa kila mwaka wa kongamano la uchumi wa dunia unafanyika huko Davos nchini Uswizi. Mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC ambaye pia ni mkurungezi wa ofisi ya kikundi cha uongozi wa mambo ya kifedha ya kamati hiyo Bw. Liu He jana ametoa hotuba ya "kusukuma mbele maendeleo ya kiwango cha juu, na kuhimiza ustawi na utulivu wa uchumi wa dunia kwa juhudi za pamoja", akieleza mkutano mkuu wa 19 wa CPC na sera za uchumi zitakazotekelezwa nchini China katika miaka kadhaa ijayo, na kusema China itahimiza kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja duniani.

  Hotuba za viongozi wanaohudhuria mkutano huo ni ajenda muhimu ya mkutano huo. Mkurugenzi mtendaji wa kongamano la uchumi wa dunia Bw. Klaus Schwab ni mwendeshaji wa mkutano huo, amesema hotuba iliyotolewa na rais Xi Jinping wa China kwenye mkutano wa mwaka jana ina maana ya kihistoria, anaamini watu wanatarajia sauti kutoka China tena.

  "Mustakabali wa China una uhusiano wa karibu na uchumi wa dunia, haswa kutokana na athari ya vitendo vya kujilinda kibiashara na uwezekano wa kutokea kwa vita ya biashara. Hivyo baada ya hotuba ya mwaka jana ya rais Xi, sasa tunafurahia kusikiliza maoni ya Bw. Liu He kuhusu uchumi wa China."

  Bw. Liu kwenye hotuba yake amesema hotuba iliyotolewa na rais Xi ilikaribishwa na jumuiya ya kimataifa, na katika mwaka mmoja uliopita, China imetekeleza mapendekezo yake kwa umakini, kupinga aina zote za vitendo vya kujilinda kibiashara, kuongeza ulinzi kwa haki miliki za kiujuzi, kuhamasisha kufanya ushindani badala ya ukiritimba, na kuongeza ufungaji wa soko la China, ili kusukuma mbele mchakato wa utandawazi wa uchumi wa dunia. Anasema,

  "Mwaka jana wakati kama huu, rais Xi alitoa hotuba maarufu ya 'kubeba majukumu ya pamoja ya kizama, na kuhimiza maendeleo ya dunia kwa juhudi za pamoja'. Kwenye hotuba hiyo, alionesha nia yake ya kuunga mkono mchakato wa utandawazi wa uchumi wa dunia na kutoa mapendekezo kadhaa kwa ajili ya kuhimiza mchakato huo. Katika mwaka mmoja uliopita, China imetekeleza mapendekezo ya rais Xi kwa hatua madhubuti."

  Bw. Liu pia amejulisha mkutano mkuu wa 19 wa CPC na sera za uchumi za China katika miaka kadhaa ijayo. Amesema uchumi wa China umeingia katika kipindi cha maendeleo ya kiwango cha juu badala ya maendeleo ya kasi, wakati huo huo China itakabiliana na changamoto tatu kuu za matishio makubwa ya uchumi, umaskini na uchafuzi wa mazingira, ili kujenga jamii yenye maisha bora halisi katika pande zote.

  Bw. Liu amesisitiza kuwa, kauli mbiu ya mkutano wa mwaka huu ni "kujenga muskatabali wa pamoja katika dunia yenye maoni tofauti", kwani nchi yoyote haina uwezo wa kukabiliana na masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa, ugaidi na mengineyo peke yake. Anasema,

  "Tunapaswa kuwa na mawazo ya kimkakati, kuongeza maelewano, masikilizano, uaminifu, na ushirikiano halisi, na kuhimiza utandawazi wa uchumi wa dunia kuendelea kwa mwelekeo wenye ufunguaji mlango, masikilizano, kunufaishana, na uwiano zaidi, kuanzisha aina mpya ya uhusiano wa kimataifa ya kuheshimiana, kushirikiana na kunufaishana na yenye haki na usawa, na kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja duniani."

  Aidha, Bw. Liu amesema China itaendelea kufungua mlango, na kusukuma mbele pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja"

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako