• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Madereva wa umma kutumia leseni mpya kuanzia machi

    (GMT+08:00) 2018-01-25 17:58:03

    Hamashauri ya kitaifa kuhusu uchukuzi na usalama, NTSA, imesema serikali itanza kutoa leseni mpya za kisasa za uendeshaji magari kuanzia mwezi Machi mwaka huu. Kulingana na meneja wa kanda ya mlima Kenya ya halmashauri hiyo Cyprian Michieka, serikali tayari imezifanyia majaribio leseni hizo mpya za kisaa na inaamini hatua hiyo italeta hali ya kimapinduzi katika sekta ya usalama barabarani nchini.

    Akiongea na wanahabari mjini Kerugoya bada ya kuwahamasisha madereva na wamiliki wa chama cha matatu cha Kukena kuhusu jambo hilo, Michieka alidokeza kuwa lseni hizo zitaanza kutolewa mwezi Machi, lakini madereva wa magari ya uchukuzi wa abiria ndio watakaozipokea kwanza.Alisema leseni hizo zina kifa kitakachohifadhi habari muhimu za dereva.

    Leseni hiyo ya kisasa ambayo inaweza kuhifadhiwa kwenye mfuko wa shati itahifadhi habari muhimu kama vile jina la dereva, kundi la damu yake na habari nyingine muhimu zikiwemo,zinazohusu ukiukaji wa sheria za trafiki.

    Kadi hiyo itakuwa na pointi 100, na iwapo zitapungua kufikia pointi 40 kutokana na makosa ya trafiki leseni hiyo itafutiliwa mbali. Dereva ataweza tu kufanya maombi ya kuongeza muda wa matumizi ya leseni yake baada ya muda wa miezi sita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako