• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Biashara zaregea hali ya kawaida baada ya safari za usiku kuanza

    (GMT+08:00) 2018-01-25 17:58:31

    Hatimae safari za usiku za magari ya umma zimeregeshwa.

    Serikali imeondoa marufuku ya usafiri za usiku wiki hii.

    Katibu katika wizara ya uchukuzi Paul Mwangi Maringa ametangaza kuwa marufuku dhidi ya usafiri wa usiku uliowekewa magari ya uchukuzi wa umma sasa zimeondolewa .

    Hata hivyo magari ya umma yametakiwa kutimiza masharti fulani kabla ya kuruhusiwa kuondolewa kwa marufuku hayo.

    Mwangi amesema wizara hiyo imekuwa imefanya mazungumzo na wadau kuhusu marufuku hayo na kukubaliana kuhusu utaratibu bora wa uchukuzi.

    Maafisa wa halmashauri ya kitaifa kuhusu uchukuzi na usalama barabarani NTSA , maafisa wa idara ya trafiki , na katibu katika wizara ya muundo msingi wamejadiliana na katibu wa wizara ya uchukuzi.

    . Halmashauri ya NTSA ilipiga marufuku usafiri wa masafa marefu wakati wa usiku mwishoni mwa mwaka uliopita kama mkakati wa kukabiliana na ajali za barabarani zilizosababisha vifo vya watu kadhaa mwezi Disemba

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako