• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda:Wachuuzi katika jiji kuadhibiwa

    (GMT+08:00) 2018-01-25 17:59:06

    Wachuuzi wanaouza bidhaa katikakati mwa jiji la Kigali na kutatiza uchukuzi kwa kuingia barabarani sasa wataadhibiwa.

    Wizara ya miundombinu nchini Rwanda imetangaza kuanza mchakato wa kuweka sheria ambayo itawawekea adhabu watu wanaovunja sheria za barabara wakitembea kwa miguu.

    Katibu wa serikali wa masuala ya usafiri Alexis Nzahabwanimana, amesema kuwa siku zilizopita waenda kwa miguu hawakudhibiwa wakati wowote wao kuvunja sheria kwani hawana sheria dhidi yao.

    Taratibu za kuweka sheria dhidi ya wanaotumia dhidi ya wachuuzi sasa zimetangazwa na hivi karibuni maafisa wa baraza wataanza oparesheni jijini.

    Aidha Nzahabwanimana amesema kwamba wapo watu wanaopita mitaani wakipiga simu na wengine wakaenda wakifika kati kati mtaani wakarudi nyuma na wakasababisha ajali au uharibifu mwingine.

    Kwa kawaida watu wanaoshikiliwa na sheria ni wale wanaoendesha magari wakiwa kwenye simu au wanoafanya makosa tofauti ambayo anakadiliwa kuwa kinyme na masharti ya kutumia barabara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako