• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania:Viwanda viwanvyoharibu mazingira kufungwa

    (GMT+08:00) 2018-01-25 17:59:29
    Viwanda villivyoshindwa kuzuia uharibifu wa mazingira sasa vitafungwa.

    KasiI ya watendaji wa serikali wakiwemo mawaziri ya kutishia kufunga viwanda vinavyokiuka sheria za mazingira, imeiibua Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, ambayo imeonya hatua hiyo.

    Katika maelekezo yake kwa serikali jana, kamati hiyo imesema serikali inapaswa kuvifunga viwanda vile tu ambavyo vitaonekana kuwa sugu katika kutekeleza sheria na kanuni za utunzaji wa mazingira na si vinginevyo.

    Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mbunge wa Mvomero, Sadick Murad alitoa maelekezo hayo baada ya Kamati hiyo kukutana na watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dodoma jana.

    Mbali ya kupitia taarifa ya utendaji wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na NEMC, pia wajumbe wa kamati hiyo walijadili kuhusu hali ya mazingira katika wiwanda na migodi nchini.

    Murad alisema baada ya majadiliano ya kina, Kamati hiyo imebariki msimamo wa serikali wa kuvitaka viwanda vyote nchini kusimamia sheria wakati wa utekelezaji wa Sera ya Ukuzaji wa Uchumi wa Viwanda.

    Alisema hata hivyo, Kamati hiyo imeona ili kuelekea katika mafanikio ya kuiwezesha nchi kuwa na viwanda vingi, ni vema kwa watendaji wa serikali na hasa mawaziri wakavifunga viwanda vile tu ambavyo vitaonekana kuwa sugu katika kutii sheria.

    Katika hatua nyingine, Mwenyekiti huyo alisema wajumbe wa kamati hiyo wameiagiza serikali kufanya ukaguzi mkubwa katika migodi nchini ambayo imekithiri katika uharibifu wa mazingira na migodi itakayobainika kukiuka sheria ichukuliwe hatua kali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako