• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Telkom ya Kenya yafuzu Fainali ya Klabu bingwa Afrika

    (GMT+08:00) 2018-01-26 09:22:12

    Timu ya mpira wa Magongo ya Telkom kutoka Kenya jana imefuzu kwa hatua ya fainali ya mashindano ya klabu bingwa Afrika yanayoendelea nchini Ghana, baada ya kufanikiwa kuwa vinara katika mechi za awali za hatua ya makundi.

    Katika mechi iliyopigwa jana, kati Telkom ilipata matokeo ya sare ya magoli 1-1 na timu ya Polisi Ghana, hivyo ikifikisha pointi 13 sawa na Kada Queens ya Nigeria inayoshika nafasi ya pili kufuatia tofauti ya wingi wa magoli.

    Telkom ambao wamekuwa mabingwa wa mshindano hayo mara tisa mfululizo, jana ilikuwa mara yao ya kwanza kudodosha pointi tangu wafanye hivyo kwa mara ya mwisho mwaka 2016 walipotoka sare ya magoli 2-2 na timu ya Chuo Kikuu cha Strathmore katika ligi kuu nchini Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako