• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Burundi wako tayari kuwa wenyeji wa mashindano ya vijana chini ya miaka 17

    (GMT+08:00) 2018-01-26 09:22:34
    Shirikisho la mpira wa miguu la nchini Burundi, limesema kuwa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 imeandaliwa vyema ili kutetea ubingwa wake wa mashindano ya Cecafa yanayotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi machi mwaka huu.

    Kuhusu maandalizi ya kuwa wenyeji wa mashindano hayo, mwenyekiti wa kitaifa wa maandalizi Mossi Yousuf amesema tayari wamekamilisha maeneo muhimu kwa ajili ya mashindano hayo.

    Akisisitiza hilo, amesema wiki chache katika mkuu wa Cecafa Nikolas Musonye alitembelea Burundi ambako alikagua viwanja na hoteli zitakazotumiwa na washiriki wa mashindano hayo.

    Akivitaja viwanja vitkavyotumika, Yussuf amesema ni Urukundo uliopo Ngozi, Umuco wa Muyinga na Uwanja wa Gitega.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako