• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Angelique Kerber avuliwa ubingwa kwenye nusu fainali

    (GMT+08:00) 2018-01-26 09:25:00
    Angelique Kerber wa Ujerumani amevuliwa rasmi ubingwa wa mashindano ya Tennis ya Australia baada ya kufungwa na Simona Halep wa Romania kwenye mechi ya nusu fainali uliopigwa jana kwa seti yenye alama 6-3 4-6 na 9-7.

    Kwa ushindi huo, Simona sasa atacheza mechi ya fainali ambapo atakutana na Caroline Wozniacki wa Denmark ambaye alimfunga Elise Martens kwenye nusu fainali.

    Kwa upande wa wanaume, Marin Cilic wa Croatia ametangulia fainali baada ya kumfunga Kylie Edmund wa Uingereza kwa seti ya 3-0 yenye alama 6-2 7-6 na 6-2, na sasa anasubiri mshindi wa mechi nyingine ya nusu fainali inayopigwa leo kati ya Roger Federer na Chung Hyeon.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako