• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Reli ya kisasa kati ya Tanzania na Rwanda kuboresha uchumi wa nchi hizo mbili

    (GMT+08:00) 2018-01-26 18:23:40

    Wafanya biashara nchini Rwanda wameitaja reli ya kisasa inayotarajiwa kujengwa na kuziunganisha nchi za Tanzania na Rwanda kuanzia Isaka mkoani Shinyanga hadi Jiji la Kigali, Rwanda ni ya mapinduzi ya kihistoria kiuchumi.

    Mapinduzi hayo yanatokana na ukweli reli hiyo itapunguza sana gharama za usafirishaji mizigo. Kwa Rwanda, inakadiriwa kuwa reli itakapoanza kutumika, itapunguza gharama za usafirishaji kwa wastani wa Dola za Marekani 1,500 (Sh milioni 3.3 za Tanzania) kwa kila kontena, hivyo kuleta unafuu wa bidhaa kwa watumiaji.Kwa mujibu wa wafanyabiashara hao, mradi huo ni wa mapinduzi kwani utarahisisha usafirishaji bidhaa, kupunguza gharama na mkombozi kwa nchi isiyofikika kupitia majini. Deus Kayitakirwa, mmoja wa wakurugenzi Shirikisho la Sekta Binafsi Rwanda (PSF), alisema reli hiyo ya kisasa itaondoa changamoto za wafanyabiashara wa Rwanda.Tamko hilo la wafanya biashara linakuja siku chache baada ya Rais John Magufuli wa Tanzania na Rais Paul Kagame wa Rwanda, kuamua kuziunganisha nchi hizi kwa reli ya kisasa ' standard gauge'.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako