• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jambojet yapanua safari zake hadi nchini Uganda

    (GMT+08:00) 2018-01-26 18:23:58

    Wadau katika sekta ya utalii wamepongeza shirika la ndege la Jambojet kwa mpango wake wa kutaka kuanzisha safari za ndege kati ya jiji la Nairobi na Entebbe kuanzia mwezi ujao. Jambojet ilitangaza rasmi kuwa itaanzisha kwa mara ya kwanza safari za ndege kati ya Nairobi na Entebbe Uganda kuanzia Februari 15. Shirika hilo litatekeleza safari mbili za ndege kwa siku kati ya Nairobi na Entebe. Mkurugenzi mkuu wa Jambojet Bw Willem Hondius amesema shirika hilo pindi litakapoanzisha safari hizo, abiria watakuwa wakisafiri kwa nauli nafuu.Wakati huo huo mwenyekiti wa chama cha watoaji huduma za hoteli tawi la Pwani Bw Sam Ikwaye amepongeza mpango huo wa Jambojet akisema hatua hito itaimarisha uchumi wa Kenya na Uganda. Aidha Ikwaye amesema hatua hiyo pia itarahisisha safari za watalii kati ya nchi hizo mbili. Kwa upande wake, mwenyekiti wa shirikisho la utalii Bw Mohammed Hersi pia amepongeza Jambojet kwa juhudi zake za kuanzisha safari za ndege kati ya Nairobi na Entebbe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako