• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bandari ya Dar es salaam yaongeza ufanisi

    (GMT+08:00) 2018-01-26 18:24:17

    Bandari ya Dar es Salaam imeongeza ufanisi kwa kupakua magari zaidi ya 600 kwa siku yakiwa tayari kukabidhiwa kwa wateja, kutoka wastani magari 150 kwa mwaka mmoja uliopita.

    Akizungumza mjini Dar es salaam, Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Freddy Liundi, amesema ufanisi huo upo pia katika mizigo mingine, yakiwemo makasha.

    Liundi amesema kwa sasa bandari yao inafanya vizuri, kuanzia upakuaji na utoaji wa makasha pamoja na magari kulinganisha na hali ya utendaji ilivyokuwa kwa miaka ya nyuma. Mwaka mmoja tu uliopita, Bandari ya Dar es Salaam ilikuwa inatoa magari 100 mpaka 150 tu kwa siku, lakini Bw Liundi anasema hivi sasa wamejipanga upya na tayari wametoa elimu kwa wafanyakazi wa kitengo cha magari, na sasa wana uwezo wa kutoa magari kwa wakati na kuwapa wateja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako